Nani Kama Mama

Mama, oh mama
Mama, oh mama eh
Nani kama mama? Ah

Oye, nani kama mama? Heshima kwa mama
Yale mateso, ulinibeba
Miezi mitisa, tumboni mwako
Pole sana mama

Nikupe nini? Heshima kwa mama, mama eh
Uliteseka siku ya kunitoa duniani
Nikupe nini? Mama, eh
Thamani ya malezi yako siwezi kuyalipa (mama eh)

Nani kama mama? (mama, mama, ma)
Nani kama mama? (mikono yako kwangu ni baraka)
Nani kama mama? (usipotoke umdharau mama, yo yo)
Nani kama mama? (ma, ma, ma, mama)

Hello mama, hii ni kwako mama
See, nimekukumbuka sana
Mom, mama, usiku na mchana
Ay, nakuombea upumzike salama

Tabia na heshima eh
Busara na hekima eh
Ay, ulinifundisha vyema eh
See, nakuombea upumzike salama

Matatizo ya dunia eh
Kweli ninayapitia
Yale ulonihusia eh
Ya kweli mama eh

Matatizo ya dunia eh
Kweli ninayapitia eh
Yale ulonihusia eh
Eeh eh, mama eh

Malezi ya mama, elimu ya mama
Haina ada wala cheti
Ila ni zaidi ya elimu ya chuo kikuu
Nikikumbuka zamani nilipokuwa mutoto
Nikilia usiku, mama, lazima utakesha na mimi

Huwezi kukubali niwe macho usiku
Nawe ufumbe macho yako
Mapenzi ya mama kwa mutoto wake
Haina mfano
Hata mapenzi ya boyfriend na girlfriend hayafiki hata robo

Nikikumbuka zamani nilipokuwa mutoto
Nikiumwa usiku, mama, lazima utakesha na mimi
Mola wasaidie wakina mama wote
Wape maisha marefu

Nani kama mama? Mama ni mama ye ye, mama ye
Thamani ya malezi yako siwezi kuyalipa
Mama, mama ye
Mama, mama, mama
Nasema mama ni mama ye
Nani kama mama? (mama)
Mama ni mama (ni mama)
Heshima kwa mama
Mama ni mama (we)

Mama, nani kama mama? (mama, mama, ma)
Nani kama mama? (mikono yako kwangu ni baraka)
Nani kama mama? (usipotoke umdharau mama, yo yo)
Nani kama mama? (ma, ma, ma, mama)



Credits
Writer(s): Christian Bope Bella
Lyrics powered by www.musixmatch.com

Link