Iyena

(Mmh) ah leo Chereko chereko chereko mwanenu nimekuaa
Zile kuringa mideko itapunguaa
Asante Mama ulinifunza nkajuaa
Baba kasema kuomba mwiko
Raha ya chumvi kununua

Tena si kwa nazi si hirizi za waganga
Kwa Baraka za baba na mama tunaduaa
Mwambie paparazi pingamizi wenye viranga
Walosema hayawihayawi yamekua (Oh oooooh)

Iyena iyena iyena iyena iyena iyena
Kwaheri tutaonana
Iyena iyena iyena iyena iyena iyena
Ntawakumbuka sana

Ooooh ndoa baraka ukipata ushukuru
Mana wanoililia ni wengi sana
Kwa watoa talaka kuitoa ni kufuru
Nimefunzwa vumilia uushinde ujana

Ili kesho mahususi kusudi wasinong'one
Embu nichumu niringe washushuke
Na hii pete ya harusi nakuvisha waone
Wakale sumu wavimbe wapasuke

Ah tena shika nanga nteke nisichomoke ndani(anameremeta)
Futa namba wablock vimada wa zamani(anameremeta)
Sio vijembe vya kanga wazi wazi mambo hadharani(anameremeta)
Hio walopanga mwenye nyumba kaja ndani(anameremeta)

Iyena iyena iyena iyena iyena iyena
Kwaheri tutaonana
Iyena iyena iyena iyena iyena iyena
Ntawakumbuka sana

Imefika tamati tulisubiri kitambo
Leo samaki kanasa kwenye chambo
Pongezi kwa kamati yanavutia mapambo
Napata picha safi litanikoma bando

Mwanamke usafii gaga kulisugua
Mume akirudi sharti viatu kumvua
Kitandani marashi massage kumchua
Kisha anzasayansi viuno kutengua

Mambo ya kuzima taa si mahaba ni kuwanga
Washa japo ka mshumaa mumeo aone shanga
(Yii) make-up kinanda kakasuti kama mbunge (anameremeta)
Mulochanga muda kujipoza na punje (anameremeta)
Humo ndani shivo amekuja na fumbwe (anameremeta)
Kula chanda ukishiba ruksa kafunge (anameremeta)

Iyena iyena iyena iyena iyena iyena
Kwaheri tutaonana (kwaheri baba mama)
Iyena iyena iyena iyena iyena iyena
Ntawakumbuka sana

Sa nataka kusasambua (sasambu)
Mi nasasambua (sasambu)
Midadi na sasambua mi (sasambu sasambua tuone)
Mguu mmoja juu (sasambu)
Usishushe chini (sasambu)
Cheza jitazame (sasambu sasambua tuone)

Aisha kimobiteli (sasambu)
Nipe za baloteli(sasambu)
Nyonga kibaskeli(sasambu sasambua tuone)
Aka kama unashika ukuta (sasambu)
Jifanye unasusa (sasambu)
Taratibu zungusha(sasambu sasambua tuonee)

Sasambu
Sasambu
Sasambu
Sasambua tuonee
Kama unawasha bajaji(sasambu)
Imwagie na maji(sasambu)
Tuwakomeshe (sasambu sasambua tuone)



Credits
Writer(s): Nasibu Abdul Juma Issaack, Raymond Shaban Mwakyusa
Lyrics powered by www.musixmatch.com

Link