Ninatamani

Nakumbuka siku unaolewa Dhahiri
Pressure wangu moyo
Maamuzi yako madhubuti ukawekeza
Na mwenye mbili moja humwacha
Hata huruma ukanitoa kafara
Kisa shida zangu kipaji mimi msanii
Mwenzangu roshan mtanashati amekamilika
Mimi hapa sina nitaanzaje nitawezaje

Ahadi ulionipa tena haina thamani
Yako maneno leo umeyafuta mwenyewe
Japo kosa langu maskini ni hoi
Ila uzuri wako bado sijasahau

Ninatamani [zako hadithi za mapenzi
Ninatamani [marashi mwilini ulivyonukia
Ninatamani [barabarani ukinishika mkono
Ninatamani [mtoto ulinitania fimbo hukusahau

Ona nivyohangaika sina mbele wala nyuma
Honey usukani umeuachia nani anipeleke
Sijazoea gear wapi niwekeze
Mwilini maumivu yamenipoza
Tena naskia umeridhia unapendeza
Ety unampenda sana kwako hodari
Tamu unampa wasiwasi umemtuliza
Penzi limekolea hata huniwazi

Ahadi ulionipa tena haina thamani
Yako maneno leo umeyafuta mwenyewe
Japo kosa langu maskini ni hoi
Ila uzuri wako bado sijasahau

Ninatamani [zako hadithi za mapenzi
Ninatamani [marashi mwilini ulivyonukia
Ninatamani [barabarani ukinishika mkono
Ninatamani [mtoto ulinitania fimbo hukusahau



Credits
Writer(s): Danson Musyoki
Lyrics powered by www.musixmatch.com

Link