Huu Mziki

Mziki umejawa majungu
Mziki umejawa fitina
Mziki bila kiki ndo kabisa wanakuzima
Mziki umejawa uchawi maana ya ushirina

Wasani Kwa wasani ndio wanaologana
Mziki umejawa timu za hao wenye majina
Ukija na ngoma Kali wanapambana kukuzima
Mziki una mashabiki tena wa kila aina
Wengi hawakujui ila wanakutukana

Eee yeah
Mziki mbona Kama huna maana
Eee yaah
Wanaologa ndio wanaojulikana
Eee yaah
Nilishakuahidi vitu vingi mama
Nipo stronger napambana
Eee yaah
Mziki mbona Kama huna maAna
Eee yaah
Wanaologa ndio wanaojulikana
Eee yaah
Nilishakuahidi vitu vingi mama
Nipo stronger napambana

Mziki una ma presenter wasiojua mziki
Ukija na ngoma kali bila pesa ausikiki
Mziki ni ushetani shabiki aeleweki
Ukitaka wakupende mpaka uimbe matusi

Mziki unapesa nyingi zaidi ya mafao ya wastafu
Lakini wanao zipata wanafanyiaga upumbavu
Wanakwenda Kwa waganga kusafisha nyota
Wanakuja shituka tayari pesa zimekwisha
Wanaanza pagawa wanaanza chachawa
Ndo maana wengine wanaishiwa kwenye madawa
Mziki na siasa hivi havikai mbali
Mziki unatumika sana kwenye kampeni
Siasa zitapokwisha mziki weka pembeni
Mziki umetumika Kama ndala za uwani

Eee yeah
Mziki mbona Kama huna maAna
Eee yaah
Wanaologa ndio wanaojulikana
Eee yaah
Nilishakuahidi vitu vingi mama
Nipo stronger napambana
Eee yaah
Mziki mbona Kama huna maAna
Eee yaah
Wanaologa ndio wanaojulikana
Eee yaah
Nilishakuahidi vitu vingi mama
Nipo stronger napambana

Mziki una mambo mengi mengine ayaelezeki
Wanaopiga picha za uchi ndo wanauza gazeti



Credits
Writer(s): Dickson Sunday Mwasomola
Lyrics powered by www.musixmatch.com

Link