Back Then

Eee ushaicheki vile uligrow up
Yaani unakumbuka amkua na kakitu
But uli have fun
Kila kitu ilikua ina bamba, haikuwa lazima ganji
Mabeste ulikua nao then uko nao sahii

Dem Days mpango ya sunday ilikua one fifty
Jam session f2 mlangoni seventy
To and fro tao, VAKO na kukunja sura
Tapi repping furu still
Shot ya moody kwa mama pima twenty
litre ya Jik, one ten
Hii ni before pulas, hii ni before naps
Steam ya nyuki ilikua down, stiiiiill
Showtime ilikua ka half time
Kutaonisha mafala kwa line na ku recharge Steaaaaam
On stage,one 2 moja, mlangoni, bouncer bubu
Redsan kwa mic, Njeri ame simama kwa meza
Crossline kutoka kwa bubu utadhani WWF
Jackie anatega akidingisha digida ka kioo
Aleki maji-imemzindia unga, ma mwaura kwa choo
Daaaaaaamn, ma stains kwa MA thirteen juu kwa juu
Itabidi toothbrush mtaani jioni
Back left kwa straight jeans ya black
Maiirungi rangi ya maini, na njugu za aparrr
Kwa socks kidunkulu kikimarinate for later
Ting badi Malo kwa hizi ten thousand watts
Mikono juu ni ka stick up, PUT YOUR HANDS UP
Vidole kadhaa walking, pori kadhaa missing
Maboys wa jamu wako charged up kwa drama
Wameclock ule conda alipeka wheels kamu last week
Niliskia kevo alichapwa manyagwenda na kamjesh
Leo ni leo, msema kesho ni ngwata Francis
Ma randevous na Osa na Ombosh blessed maizaaa
Yea back then

Nakumbuka back then (Back in the days)
Kuishi maisha pande zote mbili mdosi au maskini
Pata potea pokeah na kusherekea bila care
Mausanga za gwoko madika tembo na warembo
Nakumbuka back then, eee back in the days
Kutoka eastlando to east London hatujawai kosa mipango
Halfs mpaka ma puffs through our ups and downs
Kila wikendi ni chrisi ya kupunguza dhiki na dhambi

Ten years later msanii amedandia dush
Amevuka border,na new weather
Heart bado ya kimauru
Mm East Lando Repping North London stiiiiiiill
Bado maisha pesa pombe na anasa
Canning town club afriqueue
Hii ni before thatched House
Enzi za Simpsons na Mailbu
Just right after Lincolns na Meantime
Entry 10 Bob, Levi kwa decks
Chupa za JD mbili na choma moja
Actually ngoja make it mbili
Permy amawasili na mtu mbili
Mdreddy ametext amaanika ya tumbili kwa bendy bus bila oyster
Inspector wako area, later link up na Saimo na Kitale Club 19
Ubrisk kwa rotation, all night long kama kawa
Kwa nango's Otis yuko charr, wamekacha taxi
Mablunder zakila siku, taxi ilikua kindeeee
Amasere ticko za game ya arsenal kwa mkoba
Itabidi tumalizie club Malibu tuchapiane na oga
Ama tuenda desire kucheki K-Diplo na Nannoma
Unajua collo kwa decks itakua noma
Ama partner in crime Shasha the one na Dubwise kumalizia na reggae
Big up Cymo na sparks tunawacheki
M1 kwa tuk tuk ya Kawa, Markus kwa wheels
Davie ame bleki ka spill beer kwa back seat
Tutafika aje mtaani jo, vutia Vosti na Roba
Olipo ashakacha, kaa rada na bang'a wako area



Credits
Writer(s): Perminus Kamau
Lyrics powered by www.musixmatch.com

Link