Umenikubali

DG

Kama Mungu ungetazama
Kama watu tunavyotazama
Nisingetosha kwenye mizani
Nisingekidhi masharti
Hukuangalia historia ya familia niliyotokea
Hazikukutisha zangu tabia ulilitazama lililo Jema

Umenipenda nisiyestahili
Umeniita mwanao
Niliyejidhani ya kuwa sifai
Umenipenda upeo
Umebadilisha na yangu asili
Umenifanya mboni ya jicho lako

Mmmmmmh

Ungehitaji walio kamili
Mimi si mmoja wao
Ulichojali wangu utayari wa kufanya utakalo
Umenikabidhi na zako siri
Na kunifanya rafiki wa moyo wako

Bwana Umenikubali
Jinsi nilivyo
Umenikubali
Jinsi nilivyo
Eeeeh
Umeona jema ndani yangu
Na wala hukutazama unyonge wangu

Bwana umenikubali
Jinsi nilivyo
Umenikubali
Jinsi nilivyo
Bwana
Umeona jema ndani yangu
Na wala hukutazama unyonge wangu

Kuna muda najiuliza
Wewe ni Mungu
Wa namna gani
Uliyenipenda na kunikubali
Mtu wa namna hii
Ziko nyakati hata mimi
Napata shida kujikubali
Iweje wewe unipende
Mtu wa namna hii

Eeeeeeh

Umenipenda nisiyestahili
Umeniita mwanao
Niliyejidhani ya kuwa sifai
Umenipenda upeo
Umebadilisha na yangu asili
Umenifanya mboni ya jicho lako

Eh Bwana

Ungehitaji walio kamili
Mimi si mmoja wao
Ulichojali wangu utayari wa kufanya utakalo
Umenikabidhi na zako siri
Na kunifanya rafiki wa moyo wako

Baba umenikubali
Jinsi nilivyo
We umenikubali
Jinsi nilivyo
Eeeh Bwana
Umeona jema ndani yangu
Na wala hukutazama unyonge wangu

Baba umenikubali
Jinsi nilivyo
Umenikubali
Jinsi nilivyo
Maana
Umeona jema ndani yangu
Na wala hukutazama unyonge wangu

Asanteee
Asanteee
Baba Asantee
Asantee
We maana maana
Umeona jema ndani yangu
na wala hukutazama unyonge wangu

Asanteee
Baba asantee
Asantee
Maana maana
Umeona jema ndani yangu
Na wala hukutazama unyonge wangu

Asanteee
Asanteee
Kweli Asantee
Asantee
Baba umeona jema ndani yangu
Na wala hukutazama unyonge wangu

Kweli Bwana umenikubali
Jinsi nilivyo
Umenikubali
Jinsi nilivyo
Si kama wanadamu
Umeona jema ndani yangu
Na wala hukutazama unyonge wangu



Credits
Writer(s): Joel Lwaga
Lyrics powered by www.musixmatch.com

Link