Genge Love - Feat. Lady B

Ehh najua manze jamaa watoto sana sana wamekua waki complain
sana sana wanasema yaani
Kenyan men are very unromantic
Nasema pole
on behalf of all the men out there
Hii ni genge love
Inaenda kitu ka hii

Ntakupa jamii, ukinijalii
Nimeapaa
Uwe msanii, huna ganjii
Sitakuacha
Bora unipe unacho naahidi mgenge mi
nimeapa
Mapenzi bora yatudumu mi na wee
bila shaka

mtoto kwangu wewe ni ka maua nispokushughulikua ka kukuwekea maji naeza kuua
nashkilia roho yako fiti ka glasi nisiiachilie sabu jo, naeza ivunja
mtoto wee ni ka thambi au halua
na niko sure utamu ya manzi mnaijua
Nyuma ya kila mwanaume anaendelea kimaisha
kuna mrembo anamshkilia anam-support kabisa
Manzi wee ni ka pesa yangu kwa benki
Nakuhifadhi maisha ya baadaye watoto wengi
Siunajua wewe ni ka track noma kwa msani
Feeling yenye wee hunipa nikiwa studio ndani
Mtoto ni ka hewa ya asubuhi na mapema
Jua ikikata wingu smile yako unacheka
Saa hii una-blush unadai nakudanganya
Ukweli ni ningependa kuomba hizo mbana

Ntakupa jamii, ukinijalii
Nimeapaa
Uwe msanii, huna ganjii
Sitakuacha
Bora unipe unacho naahidi mgenge mi
nimeapa
Mapenzi bora yatudumu mi na wee
bila shaka

Mtoto wewe ni ka ndai yangu balaa
Vile mimi huishughulikia kuiekea tuu hivi ngataa
Na rangi ya power ndio ikae smattaa
Shika hii noti kuja tengeza hataa
Sura nywele shuglikia na vitu kadhaa
Ndio niringie ma boy wangu vile tu umevaa
Mtoto najua wewe ni ka paka yangu ya nyumba
Nakupapasa mgongo, nywele na sura
Matym unaeza kuwa ka simba wa Tsavo
Najua hutaki manzi mwengine karibu na boy wako
Cheki vile unatembea ka tausi
Swagger juu na Maringo nafkiria harusi
Mtoto wewe ni ka pete ile ndakuoa nayo
Itakwama kwa hii mkono wacha rungu ya nyayo
Najua hujazoea kuambiwa vitu ka hizi
genge love ndio una-experience sa hizi

Ntakupa jamii, ukinijalii
Nimeapaa
Uwe msanii, huna ganjii
Sitakuacha
Bora unipe unacho naahidi mgenge mi
nimeapa
Mapenzi bora yatudumu mi na wee
bila shaka

Mtoto wee ni ka gazeti mi huwaga nimekusoma
Ukinijamia nakuangushia joke moja noma
Nishakwambia wewe ni ka vumbi ikishakana na mvua
Inanukiaga aroma moja tu ya ki sure
Ndio wewe ma cocoa butter ukishajipaka
Mapua yangu kwa shingo tu najipata
Mtoto kwangu wewe ni ka kitunguu
Unanitoaga machozi najikausha tu vigumu
Labda waeza sema jo hii story haikubambi
Hakuna mahali naenda hapa nadunga kambi
Jah jah mwenyewe niko sure akikuona yeye hucheka
Malaika wanamgotea moral! vile alikujenga
Kuna vitu mob sana naeza ku compare nazo
Lakini hii, hii ndio mwisho ya mawazo
Wewe ni ka mstari ya mwisho kwa ngoma
Venye ina-blend fiti na inaingiza chorus ha

Ntakupa jamii Ukinijalii
Nimeapaa
Uwe msanii huna ganjii
Sitakuacha
Bora unipe unacho naahidi mgenge mi
nimeapa
Mapenzi bora yatudumu mi na wee
bila shaka



Credits
Writer(s): Hubert Nakitare
Lyrics powered by www.musixmatch.com

Link