Ulinumba Nikuabudu

Haleluya
Uliniumba nikuabudu bwana

Uliniumba nikuabudu (Uliniumba nikuabudu)
Kwa ajili yako mimi naishi (oh Uliniumba nikuabudu)
Pasipo wewe singekuwepo (oh Uliniumba nikuabudu)
Mimi ni kazi ya mikono yako (oh Uliniumba nikuabudu)

Baba ninaona nikuabudu
Maana matendo yako ni mengi sana
Ishara zako Baba ni nyingi mno
Maana wewe ndiye Mungu wangu
Uliniumba niseme matendo yako
Wewe ndiye Mungu, wa miungu eh haleluya baba
Wewe kimbilio letu na ngome yetu
Hakuna aliye kama wewe

Uliniumba nikuabudu baba (Uliniumba nikuabudu oh)
Pasipo wewe singekuwepo (Uliniumba nikuabudu oh)
Kama si wewe singeliishi (Uliniumba nikuabudu oh)
Kwa ajili yako mimi naimba (Uliniumba nikuabudu oh)

Maneno ya kusema yananikosa
Maana matendo yako ni ya ajabu
Maana ishara zako ni nyingi mno
Kwa macho nimeona makuu yako
Masikio nimesikia matendo yako
Ndio maana nimetambua
Ya kwamba niliumbwa nikuabudu
Mungu wa milele haleluya oh

Uliniumba nikuabudu baba (Uliniumba nikuabudu)
Kwa ajili yako mimi naishi oh(Uliniumba nikuabudu)
Umenipa sauti nikuimbie baba (Uliniumba nikuabudu)
Hata watu wote wanajua yeah (Uliniumba nikuabudu)

(Uliniumba nikuabudu)
Ninasema uliniumba (oh Uliniumba nikuabudu)
Wewe ni nuru ya maisha yangu baba(oh Uliniumba nikuabudu)
Wewe ni mwamba wa imani yangu baba (oh Uliniumba nikuabudu)

Haleluyah yesu
Mataifa yote ya dunia njoo tumuimbie bwana
Maana fadhili zake ni za milele
Daudi anasema hata wakati moyo wangu unakuwa na uoga
Ni kwako mungu ninajileta
Maana hakuna aliyekutumainia akapata haya

Haleluya, yesu ni mfalme (Uliniumba nikuabudu)
Uliniumba nikuabudu (oh Uliniumba nikuabudu)
Mataifa yote munisikie haleluyah (oh Uliniumba nikuabudu)
Pasipo yesu mimi singelikuwepo (oh Uliniumba nikuabudu)
Kama si yesu singeliishi oh (Uliniumba nikuabudu)
Wewe ni mwamba wa maisha yangu oh (oh Uliniumba nikuabudu)
Umeokoa wazazi wangu baba (oh Uliniumba nikuabudu)
Umeokoa taifa lako yea(oh Uliniumba nikuabudu)



Credits
Writer(s): Angela Chibalonza Muliri
Lyrics powered by www.musixmatch.com

Link