Kupendwa Raha

Kupendwa raha bwana
Hata mikunjo kunjo kwa sura imeisha
Natabasamu lanivisha ujana
Kwa raha ya penzi bwana
Nakuonaga kama maji ya bahari kwa mwili
Kuondoazo hali na shari kwa penzi eeh

Mi nimekuwa mwepesi kwako
Kusema nakupenda wewe
Kwa hapo zamani hili neno kusema
Ni mpaka niwe high high high

Nishike mkono
Nivushe ng'ambo nyingine
Nivushe o, nishike o
Tufike o pamoja

Nishike mkono
Tuvuke ng'ambo nyingine
Nivushe o, tuvuke o
Tufike pamoja

Nishike mkono nikushike twende kando
Nikukoki kijeshi we si komando
Bonge la penzi bonge la bango
Siku mzima hewani tunamaliza bando

Kwako niko huru sijihami, niko huru
Unanipa raha Bongo naiona Chicago
Unafanya wanga watulize kipato

Mahaba mengi kama mvua inayochuruza
Nishike mwili unajua kunibburudisha
Bila ya Mungu kwenye jua tungekuruzika
Leo tunatambua nani wa kushurudisha

Nishike mkono
Nivushe ng'ambo nyingine
Nivushe o, nishike o
Tufike o pamoja

Nishike mkono
Tuvuke ng'ambo nyingine
Nivushe o, tuvuke o
Tufike pamoja

Kupendwa raha bwana
Na nguo nikivaa zakaa kwa mwili
Na raha sana usoni na rohoni
Kwa lako penzi bwana siku zaenda kasi
Na wala hazigandi
Dhamani ya moyo ni si ya fukoni

Kwako niko huru sijihami, niko huru
Nimependa nawe umependa twaenda mbali
Kwako niko huru sijihami, niko huru

Nishike mkono
Nivushe ng'ambo nyingine
Nivushe o, nishike o
Tufike o pamoja

Nishike mkono
Tuvuke ng'ambo nyingine
Nivushe o, tuvuke o
Tufike pamoja



Credits
Writer(s): Judith Wambura Mbibo
Lyrics powered by www.musixmatch.com

Link