Hatia III

Ah
Nakusalimu mwafrika, nakusalimu habari gani
Nikaribishe tuketi, niseme yaliyo ndani
Sahau kuhusu hadithi za kale za upendo wako
Nataka leo tukae tuijadili kesho yako

Kutoka kupiga raml na kutii mizimu
Umeanza kufata amri za TV na simu
Na ubaya ni kwamba umeanza kuikacha sanaa
Na kufata siasa ambayo inakulaza na njaa

Na kila unachokiona unataka kubeba
Vichache vimekushinda na unapanga kuongeza
Juzuu, Katekisimu mpaka Novena
Sio zako, zako zilikuwa ni kutamba ngojera

Umezubaa, majirani wameanza kufika kwako
Na unaamini kuwa watakubebea shida zako
Kwa sababu ya ujinga, umezidi umasikini
Unamjengea jirani kwako unachimba unabaki chini

Zamani ulikuwa una sembe ya kusaza
Uliabudu kazi ukaliweka jembe kwenye shamba
Ghafla ukauza panga ukapamba jembe kwenye kabati
Ukanunua kioo ujirembe ili uende na wakati

Umechagua urembo na umetupa werevu
Umeuza mifugo, unafuga kucha na ndevu
Familia iwe mwafrika uzame mitini
Au uombe msaada wakati unakufa na fasheni mwilini

Mwafrika una mzigo mkubwa wa madeni
Hauna mali ardhi yako ni 'future ya wageni
Unalala ndani kungoja hisani ya wenye nguvu
Nyumba iko wazi wewe uko ibadani unaabudu

Ujasili ni kujimudu mwafrika haujui hili
Umejaliwa nguvu na unashindwa kuzihimili
Unavamia diplomasia.unatunga hotuba
Na hakuna mwenye hisia... kuwa upo nyuma ya muda

Ah
Unapoteza stadi za maisha
Kwa elimu ya magharibi ikuweke ofisini suti kubwa
Ukumbatie dawati la nyazifa
Huku unauwa nguvu kazi ya taifa

Umepitiliza nyumbani hauna vituo
Umekuwa mtumwa wa sera zao kiasi kwamba hauna future
Hauna dira, hauna lugha hauna nguo
Milango ya fahamu imefungwa na ufunguo

Umepewa karatasi ukaita jina pesa
Ukasubiri ikuletee furaha ikakutesa
Ukauza umoja ukauza amani ukauza utu
Ukawashusha mashujaa wako ukamwinua Yesu wa kizungu

Una kucha ndefu kushika chungu matusi
Hauwezi kuandika history haumudu herufi
Ume-bleech nywele, mdomo mwekundu umebusu baruti
Nikuite nani, mwafrika mzungu au mzungu mweusi

Ah
Unadanganywa rangi yako sio nzuri
Ili utafute pesa ukawaungishe vipuri
Ume-switch kutoka Mama Afrika mpaka drama Queen
Una nunua TV uone Afrika ikizama chini

Mwafrika umeshakosa mipango
Unajua kuchonga ngenga badala ya kuchonga vinyago
Unaacha wanyama Mikumi, Serengeti
Unasafiri unaenda kushangaa ghorofa Chicago

Unarudi unajikuta Mmarekani eti real nigga
Mbona haulili bili nigga?
Jasiri haiachi asili real nigga
Kamwe usijiite G nigga

Hauwezi kuwa warrior
Unajua majina ya wasanii kishinda historia
Unasahu mapishi.hauendi jikoni
Unakufa na ngoma mwilini cheni shingoni

Kwa heshima na taadhima unautunza Msaafu
Unatupa kitenge.kisha unafunga hijabu
Na ubaya ni kwamba bado haujajua sababu
Unapewa Zaburi utafakari mwenyewe wakichukua dhahabu

Ufeli majibu uishie kubuni
Ushindane nani msafi aende mbinguni
Mhanga wewe rudi uzipitie kanuni
Umeshikishwa kitabu wenzio wakushikie uchumi

Mwafrika hii haikuingii nikichana
Unanuka sana kiasi hauvutii kama jana
Kiburi moyoni haisikii unapokanywa
Unatia aibu.kiukweli sijivunii kuwa mwana

Na bado unaamini shahada ya shule ni zana
Haujui ukitaka ule ni shamba
Unafunga ubongo unafungua mikono ili wakupe msaada
Umesahau kuwa vya bure gharama

Mchezo wako sheria zao utashindwa
Ukiishi porini kama haiwindi utawindwa
Inasikitisha wenzako wanaigiza ili waishi
Ila we unaishi kwa kuigiza sio

Umekuwa dekio, umekubali kuwa soko la pombe
Na sigara
Soko la risasi bunduki na mabomu
Soko la madawa ya kulevya yanauwa waafrika wenzio

Soko la dini zao soko la picha za uchi
Soko la vitu kukuziba sauti
Soko la sera onevu na mifumo gombanishi
Magonjwa batiri unanunua dawa kwa kuhisi sio?
Umezagaa visingizio
Haujui akiba ndio maana unashangaa salio

Umegeuzwa kifaa cha majaribio
Imeandikwa asiyeandaa silaha ataandaa mapambio
Mwafrika

Nakupa nahau kalili
Afrika inakufa mwafrika unadharau dalili
Unasahau wito unafata mkumbo kwa dau batili
Unakumbuka kila kitu na unasahau asili



Credits
Writer(s): Edger Vicent Mwaipeta
Lyrics powered by www.musixmatch.com

Link