Asili Halisi

Jambo woteee... jambo woteee. Jambo wote.jambo wote

Jambo wote, mtu mzima nshawasili/
Na leo ntaongelea tiba za asili/
Vuteni viti kwanza, shikeni biki kwanza/
Andikeni tiba hii inahusisha mitishamba/
Yani mimea inayotumika kama dawa/
Iwe majani mizizi, maua mbegu na maganda/
Nafaka na gundi na kadhalika/
Pia mpaka matunda yanahusika/
Vilevile makundi ya vyakula mbalimbali/
Hii tiba haihusu dawa zenye kemikali/
Mbali na kukutibu au kukuweka fiti/
Hufanya na kazi ya kujenga mwili/
Na inafanya vyote hivi kwa wakati mmoja/
Hii ndo tiba mama tiba nambari moja/
Asilimia sabini ya waafrika waliitegemea/
Mapinduzi ya kisayansi yalipofika ikalegea/

Ukiangalia gharama ni ndogo au hata bure/
Kachume, kachimbe kunywa na utafune/
Na wala hazidhuru ukiyafuata masharti/
Sasa kimbembe ni kwenye dawa za hospitali/
Mzee... Hizi dawa zina bei/
Yani utateseka sana bila pay/
Mwili ukizizoea unakuwa sugu kwa dawa/
Na ukipona ugonjwa inabaki sumu ya dawa/
Kwa hiyo inakubidi ku recover mara mbili/
Kaa kijanja ndugu kaa kwa akili/
Chunguza kipi kina madhara makubwa/
Upunguze maafa na hasara zitazokuja/
Watafute wajuzi wa tiba hizi/
Sio ushamba jitafute we mswahili/
Usishikiwe akili nature imetubariki/
Imetupa chakula, mimea yenye tiba nyingi/

Wazee wetu walituambia kwamba asili imetimia/
Wao walijifunza na kuitunza miti hiyo/
Ikawatunza pia, wakajitibia magonjwa/
Umwa chochote dawa unayopatiwa unapona/
Tuwaombe watujuze na sisi/
Tujifunze kwa wingi, vyakula na miti/
(yeah) tuache majivuno na ubishi/
(kingine) tubadilishe na mifumo ya kuishi/
Miti mingi tuko nayo mitaani/
(mingi) na mingine wala haiko mbali/
Muhimu kuwa na mashamba na bustani/
Ili isipotee inatupasa kuhifadhi/
Saivi kila kitu dili, naomba nikuhabarishe/
Kuna watu wanatuibia kwa mgongo wa u herbalist/
Epuka wizi huu kwa kusaka maarifa/
Hakikisha na kizazi chako kinarithishwa/



Credits
Writer(s): Adam Seleman
Lyrics powered by www.musixmatch.com

Link