Baraka

Hebu fikiri kuhusu afya ya mwili/
Na pili, fikiri kuhusu afya ya akili/
Fikiri, huna ugonjwa huna hata dalili/
Kamili, yani uko fiti kwenye moja na mbili/
Kisha fikiri kinyume, yani turn table/
Una ugonjwa unaumwa yani you not stable/
Hata kama hujalazwa, hujatundikiwa dripu/
Lakini hauko sawa unasumbuliwa na vitu/
Au fikiri kuhusu amani uliyonayo/
Umetulia umeshiba huna njaa hupigi miayo/
Kisha waza vita. Na migorogoro/
Hadi kulala unashindwa hulitamani godoro/
Na vurugu nyingine tu ama usumbufu/
Hata bila mabomu na kushikiana mitutu/
Fikiri kuhusu uhai na pumzi unayovuta/
Kisha wazia ku die huna pumzi umekufa/

Acha kudhania baraka ni pesa na mali tu/
Usidhani baraka ni pesa na mali tu/
Acha kudhania baraka ni pesa na mali tu/
Usidhani baraka ni pesa na mali tu/
Acha kudhania baraka ni pesa na mali tu/
Usidhani baraka ni pesa na mali tu/
Acha kudhania baraka ni pesa na mali tu/
Usidhani baraka ni pesa na mali tu/

Waza kuamka salama na kufanya mambo yako/
Hakuna kukwaruzana kupigana na watu wako/
Waza mapungufu yako ambayo bado sio kikwazo/
Cha kuziba njia zako unazopita toka mwanzo/
Iwazie roho yako, kauli na matendo/
Afu waza unavyopata kwa hiyo hali na mwenendo/
Fikiri kwa utulivu kidogo/
Acha vikubwa fikiri kuhusu vitu vidogo/
Vitu kama heshima ama kuaminika/
Au kupewa nafasi ama kutambulika/
...kuwa na bega la kuegemea/
Au sikio ambalo unaweza kulielezea/
Chochote. Kile ambacho kinakusibu/
Kuwa na ndugu wawe wa mbali au karibu/
Fikiri na vingine ambavyo sijasema hapa/
Useme why unafikiri kwamba pesa ndio baraka/

Acha kudhania baraka ni pesa na mali tu/
Usidhani baraka ni pesa na mali tu/
Acha kudhania baraka ni pesa na mali tu/
Usidhani baraka ni pesa na mali tu/
Acha kudhania baraka ni pesa na mali tu/
Usidhani baraka ni pesa na mali tu/
Acha kudhania baraka ni pesa na mali tu/
Usidhani baraka ni pesa na mali tu/

Kwa kuwa hii story imenileta kwako leo/
Kuna usemi usemao pesa ni matokeo/
Tunaujua wote wewe na mimi/
Yani umefanyaje mpaka ukashika pesa/
Umeona? Baraka ni deeper kuliko fedha/
Haihitaji hata kuzama kwenye books/
Yeah, rudi nyuma kwenye roots/
Kisha acha kusema hujabarikiwa/
Yule kabarikiwa, na we umebarikiwa/
Umebarikiwa sana we fikiri yourself/
Usipime kwa noti au material wealth/
Tena kuwa msaada bariki na wengine/
Baraka zako zitazidi mara mbili/
Na hichi ndicho mi nilichobarikiwa/
Pokea baraka hii aminia...
Baraka tele...



Credits
Writer(s): Adam Seleman
Lyrics powered by www.musixmatch.com

Link