Iqra

Uwe mtulivu uwe mjuaji much know/
Shika elimu, ongeza elimu kielimu uweze grow/
Usiache kusoma waarabu wanasema iqra/
Mambo mbalimbali fahamu kwenye maisha/
Usiache dunia inabadilika kwa kasi/
Huenda unachojua leo kitashuka thamani/
Usiishie kukumbata ulichojua zamani/
Make sure unaongeza kitu kipya kichwani/
Na hata kama ni kimoja kila day/
Zingatia hakikisha hakitoki kinastay/
Maana elimu ni elimu iwe ndogo ama kubwa/
Na kama itakufaa si mzuka?/
Umepita vidato bandugu hongera sana/
Ukaipata uliyopata heko vyema sana/
Ila hiyo sio tiketi ya kusema hapo mwisho/
Usidharau nyingine, ukasema umemaliza/

Sawa una vyeti vizuri tayari umeelimika/
Lakini hujamaliza kubali kuelimishwa/
Maana elimu yako imeegemea kwa ulivyosoma/
Ulivyospecialize ndo sana vingine holla/
Elimu ni pana mwingine kasoma kile/
Ambacho akija kwako inakuwa mambo mengine/
Na bado hakimfanyi kuwa bora kukuliko/
Maana yake ni kwamba hatujatosha kufundishwa/
Each one teach one twende hivyo maisha haya/
Nijuze nikujuze hata pasipo kulipa ada/
Elimu ni bahari tuskume chombo pamoja/
Tuvuke twende mbali tusonge kwa pamoja/
Kama wewe ni intellectual haipingwi/
Sema ikipanda kichwani ni upimbi/
Nenda unapoenda kasome bukua uchoke/
Ila hata uwe nani huwezi kujua vyote/

Nipe usikivu dadaa, nipe usikivu jamaa/
Hivi ushawahi kusikia kuhusu elimu ya mtaa/
Wapo watu hawajui kitabu kinafananaje/
Ila wana maujuzi maujanja ndo mahala pake/
Kushinda hata wasomi ma degree/
Elimu ya mtaa wali pass ma ged/
Na maarifa yao yanawasaidia kuishi/
Na maisha yao wana mafanikio kuzidi/
Sikukatishi sikukati stim/
Huenda njia zao zikawa marking scheme/
Kwako, kuwa humble kwa huyu yule hapa kule/
Chunga usiwe mjinga baada ya kuanza shule/
Fika mpaka chuo faulu na uvae joho/
Ila usiache kujifunza na usikatae bro/
Shule haiishii kiwango cha madaraja/
Na haiishii kwenye milango ya madarasa/

Yeah yeah
Elimu ni popote hujaelewa rudia tena/
Kuna wengine sheria wameijulia jela/



Credits
Writer(s): Adam Seleman
Lyrics powered by www.musixmatch.com

Link