Tunamwamini Yesu (Live)

Tunamwamini Yesu
Mwana wa Mungu Pekee
Aliyetufilia dhambi zetu msalabani
Ndiye mtetezi wetu
Mbele ya Mungu pekee
Mbali na gadhabu ya kiama tumeondolewa

Tumeondolewa, Tumeondolewa
Mbali na gadhabu ya kiama tumeondolewa

Yesu ametuelekeza
Toka penye giza kuu uu
Katuonyesha mwangaza wake humu duniani
Sasa tumekomboleewa
Tumefanywa kuwa huru
Nyuma haturudi kamwe si tumeokolewa

Tumeokolewa, Tumeokolewa
Nyuma haturudi kamwe si tumeokolewa

Roho wake atuongoza
Hatua zake ni za nuru
Kweli zake twazipokea na tunazithamini
Kwa neema atuzingira
Hadi ile siku kuu uu
Japo mwovu atuandama si tumehifadhiwa

Tumehifadhiwa, Tumehifadhiwa
Japo mwovu atuandama si tumehifadhiwa

Kwa imani twamngojea
Atakapo toka juu
Tutamwona mawinguni kweli tutafurahi
Twende naye kwa kupendeza
Ufalme wake ulio mkuu
Aliyetuandalia milele tutaishi naye

Tutaishi naye, Tutaishi naye
Aliyetuandalia milele tutaishi naye

Tumeondolewa, Tumeondolewa
Mbali na gadhabu ya kiama tumeondolewa
Tumeokolewa, Tumeokolewa
Nyuma haturudi kamwe si tumeokolewa
Tumehifadhiwa, Tumehifadhiwa
Japo mwovu atuandama si tumehifadhiwa
Tutaishi naye, Tutaishi naye
Aliyetuandalia milele tutaishi naye

Tumeondolewa, Tumeondolewa
Mbali na gadhabu ya kiama tumeondolewa
Tumeokolewa, Tumeokolewa
Nyuma haturudi kamwe si tumeokolewa
Tumehifadhiwa, Tumehifadhiwa
Japo mwovu atuandama si tumehifadhiwa
Tutaishi naye, Tutaishi naye
Aliyetuandalia milele tutaishi naye



Credits
Writer(s): Alexander Mzami
Lyrics powered by www.musixmatch.com

Link