Bwana Umenichunguza

Ee Bwana umenichunguza, nakunijua
Wewe wajua kuketi kwangu, na kuondoka kwangu
Umelifahamu wazo langu, tokea mbali
Umepepeta kwenda kwangu, na kulala kwangu
Umeelewa na njia zangu zoote, e-eh
Umepepeta kwenda kwangu, na kulala kwangu
Umeelewa na njia zangu zote

Ee Bwana umenichunguza, nakunijua
Wewe wajua kuketi kwangu, na kuondoka kwangu
Umelifahamu wazo langu, tokea mbali
Umepepeta kwenda kwangu, na kulala kwangu
Umeelewa na njia zangu zoote, e-eh
Umepepeta kwenda kwangu, na kulala kwangu
Umeelewa na njia zangu zote

Maana hamna neno ulimini mwangu, usilojua kabisa bwana
Umenizingira nyuma na mbele, ukaniwekea mkono wako
Maarifa hayo ni ya ajabu, yanishinda mimi, hayadhihiriki
Siwezi kuyafikia, hayadhihiriki, siwezi kuyafikia

Maana hamna neno ulimini mwangu, usilojua kabisa bwana
Umenizingira nyuma na mbele, ukaniwekea mkono wako
Maarifa hayo ni ya ajabu, yanishinda mimi, hayadhihiriki
Siwezi kuyafikia, hayadhihiriki, siwezi kuyafikia

Niende wapi nijiepushe, na roho yako
Niende wapi niukimbie uso wako
Kama ningepanda Mbinguni wewe uko
Ningefanya kuzimu kitanda, huko nako uko
Kama nikisema hakika giza litanifunika
Giza nalo halikufichi kitu
Giza na mwanga kwako ni sawasawa

Ee Mungu unichunguze, ujue moyo wangu
Ee Mungu (ee Mungu eee)
Unijaribu, uyajuwe mawazo yangu
Eeh Mungu (ee Mungu)
Eeh Mungu (uone kama)

Uone kama niko njia iletayo majuto ndani yangu (eeh Mungu ee) eeh Mungu (ukaniongoze)
Ukaniongoze katika njia ya haki (milele) milele (maana wewe)
Maana wewe ndiwe uliye niumba (uzima wangu)
Uzima wangu (eeh Mungu ee) ee Mungu (macho yako)
Macho yako (macho yako) yaliniona kabla sijakamilika (eeh Mungu ee) ee Mungu (nimekuita)
Uisikie sauti yangu (nikuitapo Baba)
Eeh mungu (eeh Mungu ee) ee mungu (ee Mungu)

Ee Mungu (ee Mungu) unichunguze, ujue moyo wangu (ee Mungu)
Ee Mungu (ee Mungu)
Unijaribu (ee Mungu), uyajuwe mawazo yangu (ee Mungu)
Eeh mungu (ee Mungu) eeh mungu (maneno)
Maneno (maneno) ya kinywa changu (ya kinywa changu), na mawazo ya moyo (mawazo, mawazo ya moyo wangu)
Yapate (yapate) kibali mbele zako (ee Mungu)
Eeh Mungu (ee Mungu) eeh Mungu (maneno, maneno)

Maneno (maneno) ya kinywa changu (ya kinywa changu), na mawazo ya moyo (ye-iye-iye, mawazo ya moyo wangu)
Yapate (mawazo ya moyo wangu) kibali mbele zako
Eeh Mungu (ee Mungu) eeh Mungu (ee Mungu)

(Maneno) maneno ya kinywa changu, na mawazo ya moyo (iye, iye, iye)
(Mawazo ya moyo wangu) yapate kibali mbele zako
(Ee Mungu) eeh mungu (ee Mungu) ee Mungu



Credits
Writer(s): Christina Shusho
Lyrics powered by www.musixmatch.com

Link