Penzi Ni Kikohozi

Ama kweli penzi ni kikohozi kulicha huliwezi

Penzi ni kikohozi kulificha huliwez
Penzi ni kikohozi kulificha huliwez
Penzi ni kikohozi kulificha huliwez
Penzi ni kikohozi kulificha huliwez

Mapenzi yangu kwa yule kijana nikaamuwa kumfanyia mambo yote
Ili anielewe huku mimi mwenzie naumia
Jitihada zangu zote zakumfinyia jicho na kumpiga ukope
Ni kama najisumbuwa hataki hata kuniangalia
Nimetuma baruwa ya kwanza ya pili na ya tatu
Kimya moja kwa moja majibu hataki kunirudishia
Leo hii shoga yangu siri yangu nakupasulia chondechonde nishauri
Ni njia gani mi mwenzio nitayotumia

Mapenzi yangu kwa yule kijana nikaamuwa kumfanyia mambo yote
Ili anielewe huku mimi mwenzie naumia
Jitihada zangu zote zakumfinyia jicho na kumpiga ukope
Ni kama najisumbuwa hataki hata kuniangalia
Nimetuma baruwa zangu inamana hajazipata
Na kama amezipata mbona kimya yeye anijibu ae
Shoga yangu nishauri nifanye nini juu ya kijana yule
Mambo yote nimefanya hataki hatakiiiii

Kaza moyo mueleze waziwazi ujue moja
Wajuwa penzi ni kikohozi kulificha huliwezi

Kumwambia naogopa sura yangu naona haya
Sijui nifanye nini ili ajue nampenda uuuh

Kaza moyo mueleze waziwazi ujue moja
Wajuwa penzi ni kikohozi kulificha huliwezi

Kumwambia naogopa sura yangu naona haya
Sijui nifanye nini ili ajue nampenda uuuh

Kaza moyo mueleze waziwazi ujue moja
Wajuwa penzi ni kikohozi kulificha huliwezi

Akipita nashituka akisema naumia
Anapotabasamu moyo wangu unanenda mbiyo uuyeah

Kaza moyo mueleze waziwazi ujue moja,
Wajuwa penzi ni kikohozi, kulificha huliwezi

Akipita nashituka akisema naumia
Anapocheka meno yake yanan'garan'gara n'garan'gara

Kaza moyo mueleze waziwazi ujue moja
Wajuwa penzi ni kikohozi kulificha huliwezi

E jamani kina dada angalieni kina kaka wanagombania
Ngoma ngoma siyo yao yakucheza sindimba sindimba
EEH sindimba AAH sindimba
EEH Sindimba Aaah sindimba
EEH sindimba AAH sindimba
EEH Sindimba Aaah
Kumbe ni wewe ni mimi amejificha

We we we kijana we kijana unafanya nini sasa tabia gani ya
Kutesa watu bila sababu eh eh eh mwenzio anakupenda amekutumia
Baruwa chungu nzima hutaki kuzijibu kwanini? kwanini?
Unadhani wewe ndiyo mrembo pekeyako katika dunia hii ya leo?
Aah wacha wako wengi sana mjibu mwenzio aelewe moja kama hutaki ajue
Kama unataka ajue kuliko kunyamaza kitendo kama hicho ukifanyiwa wewe utasikia vizuri?
Nauliza vizuri? utafurahi kweli? ah acha maringo mpe jibu moja mwenzio



Credits
Writer(s): Fresh Jumbe Mkuu
Lyrics powered by www.musixmatch.com

Link