Malaika

AAAh Malaika wangu, fanya uje unichukue, maana - wananifuatafuata sana mh!

Malaika wangu wewe a ni wewe wakuilinda na kuitunza roho yangu isibabaishwe
Isipitiwe na upepo mbaya

Malaika wanguwe jaribu kunichukuwa uniweke ndani ya moyo wako
Wanitafute wasinione kabisa

Kwani wabaya - Wabaya
Hapa duniani - Hapa
Ni wengi sana - Sana sana tujiepushe
Vizabizabina - Wabaya
Wambea ni wengi - Hapa
Wanatuchimba - Sana sana tujiepushe
Pangu pakavu - Wabaya
Nitilie mchuzi - Hapa
Wanahangaika - Sana sana tujiepushe

Wachawi ni wengi - Wabaya
Wanga ni wengi - Hapa
Tujiangalie - Sana sana tujiepushe

Malaika - Nipokee mama
Malaika wangu we - Ninakuja
Malaika - Nipokee mama
Malaika wangu we - Ninakuja

AAh Itai nisaidie kulalamika na mizimu ya mababu Tanga Pangani Buyuni Kitopeni

Malaika wangu wewe ni wewe wakuilinda na kuitunza roho yangu isibabaishwe
Isipitiwe na upepo mbaya
Jumbe Mkuu KUngugu

Malaika wanguwe jaribu kunichukuwa uniweke ndani ya moyo wako
Wanitafute wasinione kabisa
Mti mkavu

Kwani wabaya - Wabaya
Hapa duniani - Hapa
Ni wengi sana - Sana sana tujiepushe
Kwani wambea - Wabaya
Wabaya ni wengi - Hapa
Wanahangaika - Sana sana tujiepushe
Wachawi ni wengi - Wabaya
Wanga ni wengi - Hapa
Wanatuchimba oh oh - Sana sana tujiepushe
Wambea ni wengi - Wabaya
Vizabizabina - Hapa
Wanahangaika oh - Sana sana tujiepushe

Malaika - Nipokee mama
Malaika wangu we - Ninakuja
Malaika - Nipokee mama
Malaika wangu we - Ninakuja

AAh Buyuni kitopeni, Machuwizi Mligaji ayayah
Itai! hapana kusahau kisiki cha muhingo Buyuni kitopeni

Ubaya umemrudia uuh - Umemrudia, umemrudia sasa anababaika
Ubaya umemrudia uuh - Umemrudia, umemrudia sasa anababaika
Ubaya umemrudia iiih - Umemrudia, umemrudia sasa anababaika
Ubaya umemrudia uuh - Umemrudia, umemrudia sasa anababaika

Aaaah hata kama ulikwenda Ulaya, hapana kusahau utamaduni wa nyumbani, usibadilishe mwendo
Mussa Shemtoi

Chekelea chekelea chekelea kaka - Chekelea maisha ni limoja tu
Chekelea chekelea chekelea kaka - Chekelea maisha ni limoja tu
Furahia furahia furahia wewe - Chekelea maisha ni limoja tu
Chekelea chekelea chekelea kaka - Chekelea maisha ni limoja tu
Chekelea chekelea chekelea kaka - Chekelea maisha ni limoja tu
Chekelea chekelea chekelea kaka - Chekelea maisha ni limoja tu

Mzee wa kazi Edocha Mbayao, hapana kulala tumia wakati kwa mafanikio

Itai Itai Jamaa wana usongo na mimi
Wembe ni uleule uleule na hawatakijuwa
Kilichomnyoa Kanga magoya

Wapi Mzeru, wapi Julius

Credits
Writer(s): Fresh Jumbe Mkuu
Lyrics powered by www.musixmatch.com

Link