Kaza Roho (feat. Karen)

Uwoga wangu wa kukukosa ndo unaniumiza akili.

Mi nakesha kutafuta ili nitoe mahari,

Mama wasije kupotosha Pesa ilivyo asali.

Wakatuma Vocha vocha Wakajifanya Hodari

Unga unga mwana mi inanicost

Nataka pika mboga sina carroti
Sina smart phone nataka kupost
Mi kimbilikimo wenzangu ngongoti.

Kama ahadi nishakupa nyingi

Tena maradufu

Iyo pete ka jiwe la msingi

Ishaota kutu

Nivumilie najua unataka matarumbeta
Na usilie hata tukifunga ya mkeka

Kaza kaza roho
Nadunduliza kidogo nitapata mama

Kaza kaza roho,
Robo kilo nusu tutakusanya

Kaza kaza roho
Ugali finyu kichele dona la ngama

Kaza kaza roho
Kaza roho kaza

Mmmmh
Aaahaah Uuuhm

Wanasema unanizeesha
Eti ukipata utasepa

Ila acha nikwambie we ndo kichwa

Najua ukipata nitadeka
Na kibanda chetu utaezekaa
Maana juzi mvua ilitutisha

Sidati na mawigi mwenzako
Napenda za kuchana

We umenikidhi
Busu lako ka kilo ya nyama

Bila sweta nabarizi
Joto lako lanipa salama

Yanini ulalamishi
Riziki anatoa rabana

Najua vizuri unaviona we viache tu vipite
Mwenzio mi nasaka dona

Jioni tusimeze matee
Najua unapenda nyama choma
Ila leo mi nina mkatee

Tumbo piga danadana
Ilhali kesho kukuche

Kama ahadi nishakupa nyingi

Tena maradufu

Iyo pete ka jiwe la msingi

Ishaota kutu

Nivumilie najua unataka matarumbeta
Nataka baba
Na usilie hata tukifunga ya mkeka

Kaza kaza roho
Kaza roho ohooo hooo

Kaza kaza roho
Iyee iyeeee e

Kaza kaza roho,
Nadunduliza kidogo
Nitapata mama

Kaza kaza roho
Kaza roho kaza

Iyee ie iee ie
Kaza roho kaza



Credits
Writer(s): Salum Said Nyangumwe
Lyrics powered by www.musixmatch.com

Link