Tangu Mwanzo

Tangu mwanzo, tangu mwanzo
Kisa kilichopelekea mambo yote kuvurugika
Visa tu vinajirudia
Lakini kaa ukitambua lini tangu mwanzo
Tangu mwanzo

Ukichafua husafishi
Ukiazima unachukua hurudishi
Ukipewa huridhiki
Asante kuisema hukumbuki

Ooh la la la lalala
Na ukisema unarudisha haurudishi
Unaenda moja kwa moja, kwa moja
Tangu mwanzo, tangu mwanzo

Tangu mwanzo, tangu mwanzo
Kisa kilichopelekea mambo yote kuvurugika
Visa tu vinajirudia
Lakini kaa ukitambua lini tangu mwanzo
Tangu mwanzo

Kumchunguza sana bata, kushiba itakuwa stori
Hata kosa sio kosa unataka niseme sorry
Unaleta mpaka chumbani maisha ya Insta
Ndani moyo huwezi kuweka filter

Kila siku vikao ni kama vita
Umebadilika
Ulivyokolea uliniuliza
Ufanye nini nisikuache

Ukanipa sifa nyingi nyingi
Eti kama mimi tuko wachache
Nikichelewa kurudi
Marafiki zako wanakushauri uniache

Tangu mwanzo, tangu mwanzo
Kisa kilichopelekea mambo yote kuvurugika
Visa tu vinajirudia
Lakini kaa ukitambua lini tangu mwanzo
Tangu mwanzo



Credits
Writer(s): Judith Wambura Mbibo
Lyrics powered by www.musixmatch.com

Link