Nipende

Mapenzi hayachagui kabila wala dini
Hayachagui kimo wala rangi
Hayachagui taifa
Na yalikuwepo toka zamani

Mmmh kupendwa furaha kuchukiwa karaha
Watu wanashangaa kupendwa na huyu baba
Waliochezea mapenzi leo wanajuta
Tulia na mimi nikupe nini?

Nikupe nini lady jaydee
Nikupe mahaba matamu tamu
Eeh matamu tamu

Unanipenda na nakupenda
Sijakataa tamaa
Ushiti walonitenda hapa ninakomaa lady
Komaa, achana nao, nakomaa na wewe baby

Hebu nipende we darling (Nipende)
Tuwarushe wapambe we (Tuwarushe)
Unipende we darling (Nipende)
Tuwarushe wapambe we (Tuwarushe)

Wanaona gere kuku wengi tusimwage mchele
Wanatumia ndele kutuvuruga hawatuwezi
Mi mgonjwa njoo dakitari
Chunga wasijewakakuiba hali sio shwari

Hebu nipende we darling (Nipende)
Tuwarushe wapambe we (Tuwarushe)
Unipende we darling (Nipende)
Tuwarushe wapambe we (Tuwarushe)

Usicheze cheze tu
Cheza, cheza kwa style
Usiruke ruke tu, aaah
Usicheze cheze tu
Cheza, cheza kwa style
Usiruke ruke tu
Angalia usimkanyage mwenzio



Credits
Writer(s): Judith Wambura Mbibo
Lyrics powered by www.musixmatch.com

Link