Nipe Uvumilivu

Nimekukimbilia wewe bwana
Mwamba wangu na ngome yangu
Nakuinulia macho yangu
Baba mungu naja kwako
Nainua mikono yangu juu
Nahitaji msaada wako
Nimekukimbilia wewe bwana
Mwamba wangu na ngome yangu
Nakuinulia macho yangu
Baba mungu naja kwako
Nainua mikono yangu juu
Nahitaji msaada wako
Magonjwa mengi yamenitesa
Yesu nipe uvumilivu
Dhiki nyingi zimenisonga
Baba nipe uvumilivu
Watoto wangu wanaangaika
Yesu nipe uvumilivu
Walonizalisha wamenikimbia
Baba nipe uvumilivu
Maisha yangu yamo mashakani
Baba nipe uvumilivu

Baba, baba, Mungu nipe uvumilivu
(Nipe bwana) baba, (bwana wangu) baba
Mungu nipe uvumilivu
Bwana, bwana, Yesu nipe uvumilivu
Bwana, bwana, Yesu nipe uvumilivu

Hata ndugu zangu wamenigeuka
Nahitaji faraja yako
Wamejitenga mbali nami
Nasogea kitini pako
Mbele yangu kuna giza kubwa
Ndiwe mwanga wa njia zangu
Wewe ni bwana, mume wa wajane
Yesu nipe uvumilivu
Tena wewe ni baba wa yatima
Baba nipe uvumilivu
Pia wewe ni mungu wa maskini
Yesu nipe uvumilivu

Baba, baba, Mungu nipe uvumilivu
Baba, baba, Mungu nipe uvumilivu
Bwana, bwana, Yesu nipe uvumilivu
Bwana, bwana, Yesu nipe uvumilivu

Adui zangu wamenizunguka
Wataka kuniangamiza
Wamenitegea mitego mingi
Wanawinda roho yangu
Nafsi yangu inazimia
Njoo hima nisaidie (repeat twice)

Baba, baba, Mungu nipe uvumilivu
Baba, baba, Mungu nipe uvumilivu
(Oh nakuhitaji Jehova Shama,
Wewe umeketi mahali pa juu
Wewe bwana wa wajane
Wewe Mungu wa yatima
Wewe unayeketi na maserafi na makerubi
Wewe mungu wakati wa shida zangu
Wewe uangazaye njia zangu
Oh unipendaye nakimbilia kwako)



Credits
Writer(s): Rose Muhando
Lyrics powered by www.musixmatch.com

Link