Maajabu Ya Mapenzi

Mapenzi ni kitu cha ajabu
Nitakuambia kwa nini eeh
Mimi naye tulipendana
Kama pete na kidole sijapata kuona
Siku moja aliniita akasema
Mpenzi eh nimekuwa Simwaminifu
Akaomba msamaha huku
Akilia sana mpenzi nisamehe
Nikamwambia asilie
Kwa vile nami pia mambo ni Hivyo hivyo

Usiangalie nyuma mbona
Yaliyopita yamepita
Mwambie mwenzio pole
Sitarudia tena Mungu unisaidie
Muombe samahani mwenzio
Sitarudia tena Mungu unisaidie
Maanisha unachoahidi
Sitarudia tena Mungu unisaidie

Hakuna siri tena baina yake
Na mimi ooh
Simu zake na zangu hazina
Maneno ya siri tena oh
Benki akaunti yetu ni moja
Pesa tunazitumia kwa makini oh
Furaha iko tele
Amani imejaa myoyoni mwetu Oh

Usiangalie nyuma mbona
Yaliyopita yamepita
Mwambie mwenzio pole
Sitarudia tena Mungu unisaidie
Muombe samahani mwenzio
Sitarudia tena Mungu unisaidie
Maanisha unachoahidi
Sitarudia tena Mungu unisaidie



Credits
Writer(s): Job Ndile
Lyrics powered by www.musixmatch.com

Link