Wapi Na Lini?

Nitasema ukweli uongo
Kwangu ni mwiko
Huo ndio ukweli na
Sio mtazamo
Usiniwekee maneno
Mdomoni mwangu
Hiki ninachosema
Ndicho nakiamini
Nitaanza vipi kukuzulia maneno
Utamaduni na mila
Zangu haviniruhusu
Hata kama wewe ndiwe Umenikosea
Nitakuita pembeni kule Tukayamalize

Wanasema eti mimi nimesema
Wewe na mpenzi wako mmeachana eeh
Eeh wapi na lini nimesema hayo
Eeh wapi na lini nimenena hivyo
Wanasema eti gari uendeshalo
Sio la kwako bali la kukodi
Eeh wapi na lini nimesema hayo
Eeh wapi na lini nimenena hivyo
Wanadai kuwa eti Ninakudanganya
Kama nakupenda kumbe ni Uongo ooh
Eeh wapi na lini nimesema hayo
Eeh wapi na lini nimenena hivyo

Nyosheni mikono juu
Halafu mjipepee
Cheza cheza ouh ouh
Nenguanengua ooh
Twende mpaka chini
Cheza cheza ouh ouh



Credits
Writer(s): Job Ndile
Lyrics powered by www.musixmatch.com

Link