Umenifunza

Ulo mpata anaupiga mwingi
Sio siri umenawiri
Rangi mashallah kampe hongera zake
Bato siwezi amenzidi vingi
Mwenzangu tajiri
Mi kapuku mlala njaa aah!
Sijafika level zake
Mi hali yangu pangu pakavu
Riziki yangu ndondondo
Nilicho jaliwa malavudavu
Ila kipato ndo mchongo
Mwenzangu kanizidi ubavu
Mi kijiti ye nondo
Ningewazeje kutoa madafu
Wakati mi mpera si uongo

Lakini nimemisi nimemisi kukuona kwangu
Yalaiti nami Mungu angenipa fungu langu
Labda usinge chitiii
Kama muhuni ningekuwa na vyangu
Ila atabariki nami Mungu atajibu maombi yangu

Ila umenifunza umasikini mbaya
Umenifunza umasikini mbaya
Umenifunza umasikini mbaya
Umenifunza umasikini mbaya

Na huyo ulompata usimuache
Maana anakupa nilivyovikosa mimi
Mungu awabariki fungate
Muwe wahalali awaepushie kuzini
Wala mwambie asikuchape
Aku! Mbona siku kuchapa mimi
Na we ujeuri uache
Mpe sifa mama uchunge yako ndimi
Siwezi sema nimesusa ntakuwa muongo
Kama ikitokea fursa mi bado niko singo
Hamu mwenzako kimejaa kichupa pakumwagia songombingo
Nisamehe ka mstari na uvuka
Maji yamenifika kwa shingo

Maana nimemisi nimemisi kukuona kwangu
Yalaiti nami Mungu angenipa fungu langu
Labda usinge chiti kama muhuni ningekuwa na vyangu
Ila atabariki nami Mungu atajibu maombi yangu

Ila umenifunza umasikini mbaya
Umenifunza umasikini mbaya
Umenifunza umasikini mbaya
Umenifunza umasikini mbaya



Credits
Writer(s): Abdul Hamisi Mtambo
Lyrics powered by www.musixmatch.com

Link