Turudiane (feat. Lava Lava)

Nimekuwa bubu nimepigwa na butwaa
Mdomo mzito kinywa kama ndondocha
Macho yana magugu sioni mbele najikwaa
Yani ujanja sina nimezorota
Naona! Joto si joto baridi si baridi
Mwili wa nchoma choma
Naona! Kichwa kinawaka moto
Moyo unakwenda speed
Yani homa si homa eeeeh!
Vipimo nimemaliza kwa manguri daktari
Waganga matabibu eeeh eh!
Kumbe najilimbikiza maumivu makali
Naongeza maswahibu oooh! Ooh!

Nimezunguka kote buza na yombo dovya
Sijaaambulia chochote zaidi ya kuchovya chovya
Rudi tuishi sote ujinga tu uliniponza
Jaribu kusahau yote mtima uje kuupoza
Baby fanya!

Turudiane turudiane tena
Turudiane tuwe kama zamani
Turudiane fanya turudiane turudiane
Turudiane tena unirudie baby
Turudiane tuwe kama zamani
Turudiane

Yalopita yamepita si ndwele
Rudi tugange yajayo we nimekuzoea
Tufanye yamekwisha uje tujenge ya mbele
Yale tuachane nayo mwenzako najidodea
Rudi tufunike kombe mwanaharamu apite
Tusijali tutaonekanaje kwa ndugu jamaa
Nimekubali kwako kibonde acha tu nidhalilike
Sina habari ata wakisemaje nnachotaka furaha
Yale matusi kejeli, vijembe, mafumbo kutupiana
Yote tufanye yaishe eeeeh eeh!
Najua twapendana kweli sasa ya nini tunazozana
Rudi penzi tudumishee ooooh oooh!

Nimezunguka kote buza na yombo dovya (Nimezunguruka kote)
Sijaaambulia chochote zaidi ya kuchovya chovya (Oooh oh, Oooh oh!)
Rudi tuishi sote ujinga tu uliniponza
Jaribu kusahau yote mtima uje kuupoza
Baby fanya!

Turudiane turudiane tena
Turudiane unirudie
Tuwe kama zamani Iyeeeh!
Fanya turudiane turudiane
Turudiane tena unirudie baby
Turudiane tuwe kama zamani
Turudiane



Credits
Writer(s): Abdul Hamisi Mtambo
Lyrics powered by www.musixmatch.com

Link